Klabu ya Simba bado ina matumaini ya kumbakisha kiungo wake Clatous Chama ambaye yuko ukingoni mwa mkataba wake na Wekundu hao wa Msimbazi
Mkataba wa Chama unamalizika Juni 29 lakini tayari Simba ilishafanya mazungumzo na kiungo huyo ambaye yuko kwao Zambia kwa ajili ya mapumziko
Mazungumzo ya awali hayakufikia mwafaka kutokana na mahitaji ya Chama na msimamo wa Simba kuhusu mkataba mpya
Simba imetuma maafisa wake nchini Zambia kukamilisha usajili wa winga wa Power Dynamos Joshua Mutale lakini pia wakiwa huko wanatarajiwa kuzungumza na Chama Simba ikiwa tayari kuboresha maslahi ya mchezaji huyo
Haya yote yanakuja siku chache baada ya Mo kutangaza kurejea rasmi ambapo sasa ni yeye mwenyewe anayesimamia michakato yote ya usajili
Chama ni miongoni mwa wachezaji waandamizi katika kikosi cha Simba. Katika misimu yote aliyoitumikia Simba, amebaki kuwa mchezaji muhimu
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA KITANDANI
No comments:
Post a Comment