Licha ya kupewa mapumziko ya mwezi mmoja, wachezaji wa Yanga wamepewa program maalum ya mazoezi ambayo watapaswa kufanya wakiwa makwao
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amefichua kuwa hataki kuanza tena upya pale likizo itakapomalizika
Gamondi ambaye hivi karibuni alisaini mkataba wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara, amesema wanahitaji kuwa bora zaidi msimu ujao ili kuhakikisha wanalinda kile walichonacho na kupata mafanikio zaidi
"Kila mchezaji anatakiwa kupumzika lakini hatuwezi kwenda kupumzika moja kwa moja kila mchezaji aliyemaliza msimu hapa amepewa ratiba ambayo anatakiwa kuitekeleza na kila wakati atawasilisha kwa kocha wa mazoezi"
"Hili ni muhimu sana kwa kila mchezaji kuzingatia kinyume na hapo tutakuwa wakali kwa lengo la kutokuwa na kazi ngumu kwenye maandalizi ya mwanzo wa msimu, nimeambiwa muda hautakuwa wa kutosha sana lazima tujipange," alisema Gamondi
Baada ya ratiba ya michuano ya Kagame Cup kutolewa ambapo Yanga imethibitisha kushiriki michuano hiyo inayoanza Julai 06, huenda Yanga ikarejea kambini mapema kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu 16
BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA CHUMBANI
No comments:
Post a Comment