Jemedari Said: Kibu Denis amegoma kusaini Mkataba mpya Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Jemedari Said: Kibu Denis amegoma kusaini Mkataba mpya Simba

Jemedari Said: Kibu Denis amegoma kusaini Mkataba mpya Simba

Kesho ni Simba vs Mtibwa sugar je mnyama atamaliza hasira zake usikose kuitazama mechi hii live buree kabisa kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bureee kabisa bofya sasa

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba KIBU DENIS PROSPER amekuwa akikacha kuongeza mkataba wake na Simba SC ambao unaisha mwisho wa msimu huu. Viongozi wa klabu ya Simba wamekuwa wakimbembeleza mchezaji huyo kuongeza mkataba kwa miezi 10 sasa bila mafanikio.

Awali alisema amepata ofa ya kucheza nchini Norway alipotakiwa kuleta mawasiliano ya hiyo klabu alitoa namba za wa wawakilishi ambao hawakuwa tayari kulifanya jambo hilo kiofisi na klabu ikakataa kufanya mambo kienyeji. Hali inayoaminika kwamba hao watu wanajua baada ya msimu watampata bure na Simba SC haitopata kitu. Kibu inaonekana amechagua kutokuwa loyal kwa Simba SC

Viongozi wakamuita na kukaa naye akasema mahitaji yake ili aongeze mkataba, klabu ikaridhia yote lakini bado aliendelea kukwepa kusaini mkataba huo. Viongozi wakaandaa mkataba wakambananisha baada ya kukimbiakimbia kwa muda, akasema yuko tayari kusaini ila lazima mwanasheria wake awepo, mwanasheria wake akatafutwa akaja, akasema anataka na meneja wake aje anaitwa Carlos, akatafutwa na akaja, alipoambiwa weka saini yako akasema hawezi kusaini bila kuwepo kaka yake ambaye yupo Kigoma, mchezo ukalala manake haikuwezekana kumpata kwa wakati huo.

Taarifa za uhakika ambazo Bin Kazumari inazo ni kwamba Kibu ana ofa ya mshahara wa 12M, kwa mkataba wa miaka 2 na pesa ya kusajili ya 300M (150M kwa mwaka) kutoka klabu moja ya Jiji la Dar es Salaam. Viongozi wa Simba SC baada ya kuiona hiyo ofa wakamuita kijana wao wakampa ofa nzuri zaidi lakini kijana bado amegoma kuweka kidole gumba kwenye mkataba wa klabu iliyomuweka kwenye anga za kumataifa baada ya kutoka Geita Gold, akacheza Mbeya City kabla Simba SC haijamchukua na kumpa platform ya kimataifa na kumsaidia kupata passport yake ya kwanza kama Mtanzania mwenye asılı ya Congo DR.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz