Jina la Deivi Miguel Vieira maarufu kama Gilberto raia wa Angola anaechezea Petro Atletico Luanda linatajwa kwenda kumrithi Skudu Makhudubela huko Jangwani.
Taarifa zinaeleza kuwa huenda Skudu akajiunga na Amazulu ya nyumbani kwao Afrika Kusini mwishoni mwa msimu huu hiyo ni baada ya kukosa namba kwenye kikosi cha mwalimu Miguel Gamondi.
Gilberto ni moja kati ya mawinga Bora sana ambae amekuwa akifanya vizuri na kikosi cha Petro tangu mwaka 2022 alipojiunga na timu hiyo akitokea Recreativo do Libolo ya huko nyumbani kwao Angola.
Nyota huyo anapatikana sokoni Kwa dau la USD 200,000 sawa na zaidi ya shilingi million 515 za Kitanzania.
Post a Comment