Hadi sasa Simba wamezidiwa alama (7) na Azam ingawa wana mechi mbili Mkononi lakini hata wakishinda hizo mechi zote mbili bado watazidiwa pointi (1) na Azam.
Pia ikumbukwe Simba wamezidiwa goal difference Azam wana goli (34) huku Simba wakiwa na goli (20)
Kwa kifupi Azam wana nafasi kubwa ya kushiriki CAF Champions League msimu ujao Kama watashinda mechi zao zote zilizobaki.
Ni msimu wa tatu sasa Simba wanafanya vibaya kwenye madirisha mbali mbali ya usajili,na Hali hiyo imesababisha timu kupata matokeo mabaya kiwanjani na kupoteza makombe makubwa mara kwa Mara.
Hii inawaondolea mvuto wa kuwashawishi wachezaji wakubwa na wazuri kuja kuitumikia hii timu.
Miaka kadhaa iliyopita vijana wengi wenye uwezo mkubwa wa kucheza mpira walitamani kuja Simba ili kukuza vipaji vyao na kuonekana kimataifa,kwani Simba ilikuwa imara kwenye ligi za ndani na nje,hivyo vijana wengi waliamini wakija Simba wataonekana ndani na nje ya Tanzania.
Maneno ambao Simba hawapendi kuyasikia lakini ndiyo ukweli ni kwamba timu yao kwa sasa imepoteza kabisa mvuto kwenye ligi ya ndani, na ukiangalia kimataifa Wanaelekea kupoteza hata nafasi ya kushiriki CAF Champions League….hii ni mbaya sana Kwao.
Msimu ujao wakihitaji kuşajili wachezaji wazuri nje ya Tanzania au kuwabakisha wachezaji wao muhimu viongozi watatakiwa kutumia nguvu ya ziada na Pesa nyingi ili kuwashawishi…..maana klabu yenyewe haijiuzi tena…..Mvuto unapotea Kila siku.
Post a Comment