Alicho kisema Ahmed Ally baada ya simba kuangukia nafasi ya tatu na kuhusu kucheza Shirikisho - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kisema Ahmed Ally baada ya simba kuangukia nafasi ya tatu na kuhusu kucheza Shirikisho

Ahmed Ally.

Ni kivumbi na Jasho jumapili hii ni Yanga vs Azam Fc mechi ya kibabe mechi ya kisasi ni fainali itakayo sisimua kila upande usikose kuitazama mechi hii live bureee kabisa kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayoonesha mechi hii live bure kwenye simu yako pia yale mambo yetu yale yapo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewataka mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kuacha kuidharau michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambayo wamekuwa wakiitaja kama michuano ya walioshindwa 'losers' wakidai kwamba ni kombe dogo ambalo halina hadhi.

Ahmed amesema hayo jana baada ya Ligi Kuu kutamatika huku Simba wakimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ambapo wameangukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo watashiriki msimu ujao jambo ambalo amesema hayakuwa malengo yao kabisa.

“Tumeangukia Kombe la Shirikisho ambapo hakuna Mwanasimba anayefurahi kwenda kushirki Kombe la Shirikisho, lakini hatuna budi kuliheshimu kombe hilo na kuwekeza nguvu zaidi ya kwenda kufanya vizuri katika michuano hiyo.

“Kila Mwanasimba alitamani kuiona timu yake ikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu ni mashindano makubwa na ndiyo hadhi yetu na ni fahari yetu pia kushiriki michuano hiyo, lakini bahati mbaya imekuwa kinyume chake na tumeenda kushiriki kombe la shirikisho.

“Kwanza kila Mwanasimba anatakiwa kuheshimu shindano hilo ili kuheshimu nafasi ya kufanya vizuri shindano hilo. Tusiseme tu ni Kombe la Shirikisho halafu tukaishia hapo, lazima tujiandae, sio kombe la kawaida kawaida, wapo wakubwa wa kombe hilo kama Berkane, Pyramids, USM Alger ambao ukienda kichwa kichwa unaweza kuishia pabaya.


“Niwaombe Wanasimba hata kama tunalichukia Kombe la Shirikisho hatuna budi kuliheshimu na kufanya maandalizi makubwa ili twende tukafanye vizuri kwenye kombe hilo. Aibu itakuja pale unakwenda Kombe la Shirikisho nalo unashindwa kufanya vizuri.

“Ukienda Shirikisho ukafanya vizuri unatoa ujumbe kuwa mimi hadhi yangu ni Ligi ya Mabingwa lakini kwa bahati mbaya nimekuja Kombe la Shirikisho.Tuache stori za kipuuzi na za wapuuzi kwamba ni kombe dogo, ni kombe ambalo tunapaswa kuingia kwa heshima kubwa, tukicheza vijana watatudhalilisha ukweni," amesema Ahmed.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz