Ahmed Ally: Yanga ni bora kuliko Simba, ubingwa kwetu ni mgumu - EDUSPORTSTZ

Latest

Ahmed Ally: Yanga ni bora kuliko Simba, ubingwa kwetu ni mgumu

Ahmed Ally.

Ni Simba vs Tabora united leo usikose kuitazama mechi hii live buree kabisa kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bureee

Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally amekiri kuwa mpinzani wake Yanga ana spidi kubwa na ubora wa hali ya juu na hadondoshi pointi kizembe kama Simba, hivyo kupata ubingwa mbele ya Yanga ni vigumu mno.

Simba kwa sasa watapambania nafasi ya pili ili waweze kushiriki Klabu Bingwa Afrika msimu ujao baada ya Yanga mwenye alama 65 kubakisha michezo mitatu tu atangaze Ubingwa huku akiwa na mechi 5 mkononi wakati Simba akiwa nafasi ya tatu na alam 50.

“Ubingwa kwa sasa ni mgumu, ukiangalia spidi ya ubora wa mpinzani wetu aliokuwa nao hivi sasa. Ukiangalia unaeshindana naye hadondoshi pointi kama wewe unavyodondosha, kwa hiyo unakiri ya kwamba ubingwa ni mgumu.

“Lakini tumesalia na mechi kadhaa mkononi, tunao wajibu wa kushinda mechi zetu ili baada ya mwisho hapo tuone ngoma imekuwa ngumu ama tumeambulia kitu gani,” amesema Ahmed.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz