CODE X 2: THE DIRTY GAME
CODE X 2: THE DIRTY GAME
01
"Mkuu Marine base 71 imepata tatizo" aliigia Hansen huku akihema katika ofisi kubwa za CIA Marekani, "unasemaje wewe?" aliinuka huku akifoka Ms Helen. "Ndio taarifa tulizozipata muda huu na inasemekana mmoja kati ya wale vijana ambao wapo katika project inayoendelea ametoroka" Hansen aliongea huku akijiweka sawa. "Shit bila shaka huyo atakuwa Project 75" aliongea Ms Helen aliongea huku akijishika kiuno, "hebu waambia wawakague halafu watuambie ni yupi ambae ametoroka" alimaliza kuongea na Hansen akatoka.
Ms Helen alikaa kwenye kiti chake na kushusha pumzi kwa nguvu, maana aliwaza awaambie nini wakubwa wake. Robo saa Hansen alirudi tena huku akiwa na huzuni, "wala hujakosea, alietoroka ni project 75" aliongea Hansen. "Hapo ndio kwenye tatizo kubwa maana unafahamu mara ya mwisho alivotoroka ilituchukua mwaka mzima mpaka kumkamata" Ms Helen aliongea huku akikuna kichwa, alionesha kuchanganyikiwa. "Na kipindi kile alikuwa na miaka kumi na tatu tu, sasa saa hivi ana miaka kumi na nane unadhani tutafanyaje na ikiwa ataendelea kukaa uraiani itakuwa hatari kwetu sisi" aliendelea kuongea Ms Helen huku akionyesha kukata tamaa. "Sasa tunafanyaje mkuu" Hansen aliuliza, "wewe nenda kaendelee na mambo mengine" Ms Helen alijibu na Hansen akaondoka.
"Habari bosi kuna tatizo huku limetokea, naomba kesho asubuhi nije kuonana na wewe" Ms Helen alitoa simu yake na kupiga. Baada kukata simu alibeba begi yake na kutoka ofisini, siku hiyo ilikuwa imeharibika kabisa hata hamu ya kufanya kazi iliondoka kabisa.
**********************************
Jitihda za kuzima moto ambao ulikuwa ukiendelea kuitekeketeza Marine Base 71 ziliendelea huku wakijitahidi kuuzuia moto huo usisambae sehemu nyingine. "Mkuu tuna tatizo kubwa, project 75 ametoroka" sajenti Louise aliongea, "ah huyo dogo anatabu sana, tuma boti sita ndogo zifanye msako atakua hajafika mbali" General David alijibu na kutoa amri ziachie boti kadhaa kwa ajili ya kumtafuta project 75. Sajent Louise aliondoka na kuelekea kwenye vikosi maalum vya msako, alitoa amri hio boti sita ziliingiz kazini kumsaka kijana machachari na hatari kuliko wote na hakuwa mwengine bali ni project 75.
Muda uliyoyoyoma lakini haikurudi hata moja, muda ulizidi kukatika bila kuwepo kwa mawasiliano kati ya wale walikwenda kumtafuta na kambi yao. "Vipi kuna majibu yoyote" aliuliza General David wakati akiingia ofisini kwa na kumkuta sajent Louise huku akiwa amejiinamia. "Habari ni mbaya tu mkuu, nimefanya vile ulivonambia lakini, umepita muda mrefu bila mawasiliano na wale waliokwenda, ndio nikaamua kutuma kikosi kingine kwenda kuangalia lakini wamerudi na boti tano zikiwa na miili iliotapakaa damu halafu mafuta ya boti hizo zote yalikuwa yamekwisha" alijibu sajent Louise.
"Dah huyu kijana ana balaa kwa kweli," sawa wacha niwasiliane na makao makuu niwape taarifa za kutoweka kwa Project 75" aliongea General David na kwenda moja kwa moja kwenye mkonga wa simu ambao ulikuwa umewekwa pembeni. "Hali ni mbaya kwa kweli, na alietoroka ni Project 75" aliongea kwenye mkonga huo na baada mangezi machache alikata simu na kukaa kwenye kiti chake huku akiwa ameshika kichwa asijue nini la kufanya. Jitihada za kuuzima moto huo zilifanikiwa lakini ulichukua muda mrefu sana hivyo vitu vingi viliteketea. Wanajeshi kwa pamoja walisaidiana kutoa mabaki ya vitu vilivyoungua.
Marine Base 71 ni moja kati ya kambi kubwa za siri ambazo hazijulikani na raia wa kawaida, ni miongoni mwa kambi ambazo kunafanyika uchunguzi juu ya swala zima la kuweza kuzalisha wanajeshi ambao watakuwa na uwezo kuliko kawaida. Kambi hii ipo katika kina kirefu sana cha maji katika kisiwa kimoja miongoni mwa visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Pacific. Kwa jumla kambi kama hiyo zipo zaidi ya kumi lakini hii ndio ilikuwa kubwa kuliko zote. Na serekali imeamua kufungua kambi hizo kwa siri baada ile kemikali aina ya Cindrex ootliviaso deca endroline X (CODE X) kugundilika baada ya aliekuwa mtu wa kwanza kuitengeza kupoteza ushahidi kabisa ili isiendelee kutumika.
Mwanasayansi huyo aliejulikana kwa jina la Melinda alipoteza ushahidi juu ya kemikali hiyo baada kugundua madhara itakayosababisha ikiwa itaingia mikononi mwa watu wabaya. Lakini kama ilivyoada ya wanasayansi kutokubali kushindwa jambo, walianza kufanya uchunguzi tena kupitia nakala maalum waliopewa na mwanasayansi ambae alimsaliti Melinda na kuuza uchunguzi huo. Kazi haikuwa rahisi katika kufanikisha hilo lakini walijitahdi kadiri ya uwezo huku wakiahidiwa donge nono ikiwa wataitengeza tena. Na ndipo mwanasayansi mmoja anejulikana kwa jina la Dr Hudson alipofanikiwa kuitengeza tena kwa mara nyingine.
(siku tatu baadae)
Watu wengi walionekana kukusanyika katika eneo moja kweny fukwe za bahari, walionekana kushangaa kitu fulani na minong'ono ya hapa na pale iliskika. "Hebu mguse labda ni mzima", "hapana usimguse sasa hivi gari ya wagonjwa itafika kumchukua", walisikika watu wakiongea huku kila mmoja akiongea la kwake. Dakika moja mbele gari ya wagonjwa ilifika na bila kuchelewa walishuka na machela kwenda mpaka alipo mlengwa. Kwa uangalifu na tahadhari ya hali ya juu walimnyanyua na kumuweka kwenye machela kisha wakaelekea kwenye gari na safari ya hospitali ikaanza.
Kutokana na sheria zinavosema kuwa gari ya wagonjwa ikiwa inapita gari nyingine zote zinatakiwa kukaa pembeni kuipisha. Robo saa walikua washafika hospitali, kitanda kilishushwa kwenye gari na kukimbizwa wodi ya wagonjwa mahututi. Madaktari walifika na kuanza kutoa huduma, kutokana na chumvi shati ilikuwa imegandana na mwili hivyo ilibidi ichanwe lakini kwa umakini wa hali ya juu. "Bado moyo wake unapidunda lakini katika kasi ndogo sana" daktari mmoja aliongea, walimpatia huduma za haraka ili kuhakikisha wanaokoa maisha yake. "Doh sijawahi ona binaadamu mwenye roho ngumu kama huyu" aliongea daktari mmoja huku akiwapongeza wenzake kwa kazi nzuri waloifanya, "wakushukuriwa ni Mungu kwa kweli" alijibu daktari mmoja wa kike.
****************************
"Je kuna taarifa zozote za kuonekana pahali Project 75" Mr Clinton aliuliza, "mpaka sasa hatujapokea taarifa zozote, huenda akawa amezama baharini labda" alijibu Rodriguez, "hahaha unadhani atakufa kirahisi kiais hicho, sisi tusubiri tu maana hata bila kumtafuta atakuja mwenyewe kwetu" alijibu Ms Helen. "Acheni kubishana ujinga nyinyi, mnadhani ni jambo la kukaa tukabishana wakati tunaelewa wazi kuwa akirudi huyu kijana basi maisha yetu yatakuwa hatarini" alifoka Mr Clinton, na wote wakanyamaza kimya. "kesho kutakuwa na kikao cha dharura kuhusu huyu Project 75, wote mnatakiwa mufike, haya tawanyikeni" aliendelea Kufoka Mr Clinton.
Post a Comment