Mkataba wa Saido unasema lazima aanze kikosi cha kwanza - EDUSPORTSTZ

Latest

Mkataba wa Saido unasema lazima aanze kikosi cha kwanza

Saido Ntibazonkiza

Usikose kuitazama mechi ya Simba vs Singida Black stars live bure mechi ya ligi kuu tz bara bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii mubashara bure yaani utaitazama mechi hii live bure kupitia simu yako bofya sasa

Taarifa kutoka chanzo kilicho karibu na kiungo mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza zinaeleza kuwa, mkataba wa mchezaji huyo una kipengele cha kwamba lazima aanze kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.

Kumekuwa na maneno mengi kutoka kwa mashabiki wakihoji kuwa, kwa nini kocha Benchikha amekuwa akimpanga kila mechi licha ya kuonesha kiwango kibovu na kukosa mabao ya wazi?

"Katika makubaliano ya kimkataba kati ya kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza na mwajiri wake Simba SC kuna kipengele ambacho alikubaliana na viongozi kuwa ni lazima acheze kikosi cha kwanza. Tofauti na hapo labda awe majeruhi au anatumikia adhabu ndo hatopangwa kikosini," kimesema chanzo hicho.

Saido ambaye ni raia wa Burundi, aliitumikia Yanga kwa msimu mmoja na nusu kabla ya kwenda Geita ambako alicheza nusu msimu kisha kujiunga na Simba SC. Kabla ya hapo, Saido amewahi kuzitumikia timu kadhaa za Ulaya zikiwemo za Uingereza, Ufaransa na Hispania.


Je, unafikiri ni sahihi kwa timu kuweka kipengele kama hiki katika mikataba yao?

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz