Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Young Africans, Stephane Aziz Ki ametoa ahadi kuwa mchezaji yeyote wa timu hiyo atakaefunga bao dhidi Mamelodi Sundowns atampatia kiasi cha pesa za Tanzania shilingi milioni moja.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe akifikisha salam za wachezaji kwa mashabiki zao kuelekea mchezo wao wa mkondo wa pili wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa kesho katika Dimba Loftus Versfeld nchini Afrika Kusini.
Kamwe amesema kuwa, Aziz Ki pia ameahidi kwa upande wa mabeki iwapo watazuia vizuri bila kuruhusu goli, atapatia Tsh milioni 1.
Hii inaonesha kuwa sio mechi ya viongozi tu bali hata wachezaji wenyewe wanaitaka mechi na wana shauku ya kupata ushindi.
Amesema Ally Kamwe,
No comments:
Post a Comment