KIKOSI cha Yanga SC jana Machi19 kimeingia kambini, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya nyumbani na ugenini Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPAz
No comments:
Post a Comment