Baada ya kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa kibabe kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy, kikosi cha Simba sasa kinhamishia makali yake kwenye ligi kuu ya NBC
Mnyama anautaka ubingwa msimu hivyo ni wazi kila atakayekuja mbele anapaswa akabidhi alama zote tatu kwa wababe hao wa Kimataifa
Kazi inaanza Jumatano March 06 mkoani Morogoro kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa uwanja wa Jamhuri
Ratiba itaendelea kwa mechi mfululizo ambazo zitakuwa zikipigwa kila baada ya siku tatu
Baada ya Prisons watakaoufuata ni Coastal Union (ugenini) na mechi mbili dhidi ya Singida FG na Mashujaa ambazo zitapigwa uwanja wa Jamhuri
Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 36 lakini pia ikiwa na mechi nne za viporo
Yanga bado inaongoza na alama 43 sawa na Azam FC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment