Mechi za kukamilisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa zilipigwa jana na sasa kinachosubiriwa ni droo ya robo fainali itakayofanyika huko Misri
Timu zilizomaliza nafasi ya kwanza katika makundi yao ni Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas, Petro Atletico na Al Ahly wakati TP Mazembe, Simba, Esperance na Yanga zikimaliza katika nafasi ya pili katika kila kundi
Katika droo ya robo fainali timu zilizomaliza nafasi ya pili zitapangwa dhidi ya timu zilizomaliza vinara katika makundi tofauti
Kwa maana Yanga itapangwa dhidi ya kinara wa kundi A, B au C yaani Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas au Petro Atletico
Mechi za robo fainali mkondo wa kwanza zinatarajiwa kupigwa mwishoni mwa mwezi huu Yanga ikianzia nyumbani na kumalizia ugenini
No comments:
Post a Comment