Mwandishi nguli wa habari za michezo barani Afrika Mamadou Gaye amezungumza na PitchSide Podcast ya Mamelodi na kwenye mazungumzo hayo ,amewapa tahadhari Mamelodi kuelekea mechi yao dhidi ya Yanga
Mamadou ametaja baadhi ya sababu ikiwemo ya Yanga kutoka kupoteza kwenye mechi yao ya mwisho dhidi ya Azam FC hii imewaongezea umakini lakini pia kucheza fainali kwenye CAF CC msimu uliopita kunawapa shauku ya kufanya vizuri kwenye CAF CL
“Kama wameweza kucheza fainali ya CAF Confederation Cup kwanini washindwe kucheza Nusu Fainali ya CAF Champions League “
“Kama Mamelodi itajisahau basi itashangazwa “
No comments:
Post a Comment