Kwa takwimu hizi, Yanga wakishinda kwa Mkapa tu kazi kwisha! - EDUSPORTSTZ

Latest

Kwa takwimu hizi, Yanga wakishinda kwa Mkapa tu kazi kwisha!

Yanga wakishinda kwa Mkapa tu, wamemaliza kazi

Zimebaki siku chache bonyeza hapa kudownload app yetu mapema ili uweze kutazama mechi ya Simba vs Al ahly na Yanga vs Mamelodi live bureeeee kabisa bonyeza kuidownload mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi yaani mechi unaitazama kupitia simu yako bureee

Klabu ya Yanga itashuka dimbani kukipiga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi ijayo Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Iwapo Yanga watashinda nyumbani kwa ushindi wowote ule watakuwa na uwezekano mkubwa sana wa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Hii ni kwa sababu Mamelodi Sundowns huwa hawana matokeo mazuri wakiwa kwao iwe katika dimba la FNB Stadium au Loftus Versfeld hasa kwenye hatua ya mtoano.

Mara nyingi Mamelodi Sundowns wametolewa nyumbani kutokana na matokeo ya ugenini.

Mwaka jana bao la kujifunga la Mothobi Mvala liliwapa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Wydad Ac na kuishia nusu fainali baada ya kupata suluhu (0-0) ugenini.

2021/2022 Petro de Luanda alimtoa Mamelodi Sundowns palepale nyumbani kwake baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Petro kusonga mbele kwa jumla yaushindi wa mabao 3-2 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani

2021/2020 Al Ahly alimtoa Mamelodi Sundowns nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-1 baada ya kupata ushindi wa 2-0 Cairo. (alirudia alivyofanya 2019/2020)

2019/2020 Al Ahly alimtoa Mamelodi Sundowns nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-1 baada ya kupata ushindi wa 2-0 Cairo.

2019/2018 Mamelodi Sundowns alipasuka 2-0 ugenini dhidi ya Wydad akaenda kushinda 1-0 nyumbani na kutolewa.

2017 Mamelodi alifungwa 1-0 ugenini dhidi ya Wydad na kushinda 1-0 nyumbani kisha wakatolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Hata kwenye AFL Mamelodi alivuka hatua ya robo fainali baada ya kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Petro de Luanda na kutoa suluhu (0-0) nyumbani.

Kama Yanga watashinda ushindi wowote ule hapa nyumbani watakuwa na uhakika wa asilimia kubwa kusonga mbele.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz