Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ndiyo wapinzani wa Yanga SC kwenye Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sundowns mpaka sasa ndiye kinara kwenye msimamo wa ligi kuu ya nchini humo akiwa amecheza michezo 18, ameshinda 14, sare nne, hajapoteza mchezo na amekusanya alama 46 pia amewazidi alama 13 na 'anaviporo' viwili nyuma ya wapinzani wake kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Tuangalie takwimu zake za jumla katika michuano yote anayoshiriki msimu huu ikiwemo ligi kuu, Sundowns pia wameshiriki MTN8 Cup, Nedbank Cup na Ligi ya Mabingwa Afrika na kutika mashindano hayo wamecheza michezo 25, wamefungwa mechi 4, sare 7 na wameshinda mechi 14.
Mamelodi Sundowns sasa wanatarajia kutua nchini kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Yanga SC kwenye #CAFCL na mara ya mwisho wawili hawa walikutana Jumapili ya tarehe 27, May 2001 katika Dimba la CCM Kirumba Mwanza na matokeo yalikuwa sare ya 3-3.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment