Gamondi: Nimewafundisha Mamelodi, sina presha ila....! - EDUSPORTSTZ

Latest

Gamondi: Nimewafundisha Mamelodi, sina presha ila....!

Kocha Gamondi.

Usikose kuitazama mechi ya Azam fc vs Yanga live bure kupitia simu yako Bonyeza hapa kudownload app yetu inayorusha mechi zote mubashara bure unachotakiwa kuwa nacho ni mb za mia tano tu bonyeza hapa sasa

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya soka ya Yanga imepangwa kumenyana na Memolodi Sundown ya nchini Afrika Kusini kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi anafurahi kukutanishwa na timu yake ya zamani ambayo inacheza soka kama lao akisema sasa ni wakati muafaka kwa Yanga kukaa meza moja na timu kubwa Afrika.

“Ni timu yangu ya zamani, tuliwa mabingwa mwaka 2006 nikiwa na Mamelodi, nilikuwa na wasaa mzuri wa kuifundisha timu hiyo. Nina furaha kucheza Mamelodi kwa sababu ni timu ninayoipenda. Kama ulikuwa sehemu ulifanya jambo zuri, lazima hisia zitaendelea kukujia."

Amesema kwa timu yenye malengo ya kuwa miongoni mwa timu tano bora barani Afrika ni lazima ni ishindane na wakubwa, kwahiyo hiki kitakuwa ni kipimo tosha kwao na kwa soka la Tanzania kiujumla.

“Mamelodi ni timu kubwa na wanacheza soka kama lile tunalocheza sisi, ninadhani kwa Yanga ni wakati mzuri wa kupambana na timu kubwa. Nilikuwa nambwambia Rais (Eng. Hersi Said) kwamba, kwa sasa Yanga inakaa meza moja na timu kubwa, tukiwa na malengo ya kuwa kwenye top 5 ya Afrika lazima tupambane na hawa wakubwa.

“Hii itakuwa sehemu sahihi ya kupambana na kujaribu kuonesha uwezo wetu. Mimi nimefurahishwa na soka la Tanzania, sio Yanga tu hata Simba, timu zote hizi mbili zinaiwakilisha vizuri Tanzania kwenye soka la Kimataifa. Taifa linaonesha kukua kwenye tasnia ya soka. Watanzania wanatakiwa kutembea kifua mbele.

“Ukilinganisha bajeti ya Mamelodi na Yanga ni vitu viwili tofauti, wao wamekwenda kuchukua mchezaji Argentina kwa dola milioni 4 wakatri sisi tunamchukua Okrah kwenye dirisha dogo tena bure.

“Kwa timu yetu kitu ambacho bado ni uzoefu kwenye mashindano makubwa, utaona hata mechi yetu hdidi ya Al ahly tulifungwa sababu ya uzoefu tu, tulifanya kosa hapa tukafanya kosa kwao. Soka ni mchezo wa makossa, lakini sisi tukop tayari kwa ajili kupambana na Mamelodi, kila kitu kinawezekana kwa nini tushindwe?"

Je, akifanikiwa kuwatoa Mamelodi, anajiona akifika fainali? Gamondi anasema; “Siwezi kuzungumzia kwamba tukimtoa Mamelodi tuna uhakika wa fainali, soka haliko hivyo.

“Mimi ni kocha ninayeamini katika mpango wa kila hatua, tumepambana kwenye makundi tukatoboa kwa sasa tupo kwenye robo fainali, hivyo tunaandaa mpango kwa ajili ya robo fainali na baada ya hapo tutaona hatua inayofuata kama tutafanikiwa kufika,” amesema Gamondi.

Gamondi anatoa tahadhari kwamba hakuna haja ya kuwakabili Mamelodi kwa presha ya kulazimisha ushindi kwa kuwa wao wameshazoea kucheza hatua hii; “Tukiwatoa ni mafanikio makubwa kwetu, lakini tusipowatoa pia tutakuwa tumepata uzoefu mkubwa,” amesema Master.

ROBO FAINALI Simba SC vs Al Ahly TP Mazembe vs Petro Atletico Esperance vs ASEC Mimosas Yanga SC vs Mamelodi Sundowns

NUSU FAINALI Esperance/ASEC vs Yanga/Mamelodi TP Mazembe/Petro Atletico vs Simba/Al Ahly.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz