Azam FC wafafanua ishu ya James Akaminko - EDUSPORTSTZ

Latest

Azam FC wafafanua ishu ya James Akaminko

James Akaminko

Yanga vs Mamelodi, Simba vs Al ahly unaanzaje kukosa mechi hizi za kibabe bonyeza hapa kudownload app yetu uweze kutazama mechi hizi zote live bureee kabisa bureeee bofya sasa kuidownload app mapema ili kuepuka usumbufu

Meneja wa habari na mawasiliano Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kusimamishwa kwa kiungo wa timu hiyo James Akaminko kwasababu ya utovu wa nidhamu.

Juzi kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yao na Yanga, timu hiyo kupitia ukurasa wa Instagram ilitoa taarifa ya wachezaji watakaoukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali ambapo kwa upande wa Akaminko ilielezwa kuwa ana adhabu.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Zaka amesema kuwa taarifa hizo si za kweli kwani wanaosambaza walitafsiri vibaya neno ‘suspended’ na kwamba kukosekana kwa mchezaji huyo kwenye mechi hiyo kulitokana na kuwa na kadi tatu za njano ambapo kikanuni hakuruhusiwa kucheza.

“Kumekuwa na taarifa mitandaoni kwamba kiungo fundi wa Azam FC, James Akaminko, amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu. Taarifa hizi siyo za kweli hata kidogo.”

“Wanaosambaza walitafsiri vibaya kutoka chapisho rasmi la Azam FC kupitia Instagram kuelekea mchezo wetu dhidi ya Yanga.”

“Kilipotajwa kikosi, yaliorodheshwa majina ya wachezaji wote, waliopo na wanaokosekana pamoja na sababu zao”.

“Kwa fundi James Akaminko pakaandikwa SUSPENDED, ni kwamba James Akaminko alisimamishwa na kanuni za ligi kutokana na kuwa na kadi tatu za njano hivyo kuukosa mchezo dhidi ya Yanga.”

Ameongeza kuwa baada ya mchezo huo, ndipo adhabu ya James ilipoishia na hivyo atakuwepo kwenye michezo mingine endapo atakuwa sawa kimwili na kiakili.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPAz



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz