Shirikisho la Soka Africa CAF limetoa orodha ya viwango vya ubora wa vilabu Africa ambapo Klabu ya Yanga imepanda kutoka (18) hadi nafasi ya (11) kwa msimu wa 2024/25.
Kiwango cha klabu kinapanda kutokana na mafanikio yake katika mashindano 2 vilabu vya CAF; Ligi ya Mabingwa wa CAF na Kombe la Shirikisho la CAF.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Timu inayopokea pointi zaidi katika msimu uliopita itachukuliwa kuwa timu iliyo kwenye nafasi ya juu. [13]
Vilabu vilivyoorodheshwa kwa Ligi ya Mabingwa ya CAF 2024-25 na Kombe la Shirikisho la CAF 2024-25 itatokana na matokeo kutoka kwa kila shindano la vilabu la CAF kuanzia 2019-20 hadi msimu wa 2023-24.
01. Al-Ahly - Alama 72
02. Wydad Athletic - Alama 55
03. Mamelodi Sundowns - Alama 49
04. Esperance de Tunis - Alama 46
05. Petro de Luanda - Alama 39
06. Raja Casablanca - Alama 35
07. TP Mazembe - Alama 33
08. Zamalek - Alama 33
09. RS Berkane - Alama 32
10. CR Belouizdad - Alama 32
11. Young Africans - Alama 31
12. USM Alger - Alama 31
13. ASEC Mimosas - Alama 30
14. Simba SC - Alama 29
15. Pyramids - Alama 29
16. JS Kabylie - Alama 22.
CR Belouizdad imeporomoka kutoka (7) hadi (10) baada ya kushindwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya CAFCL huku timu zilizofuzu robo fainali zikisogea juu ikiwemo Yanga, TP Mazembe, ASEC na nyingine.
Simba SC imeshuka licha ya kwamba inayo nafasi ya kurejea top (10) endapo itafanikiwa kuingia robo fainali atafikisha points (39) katika nafasi ya (6).
Msimu wa (21/22) Klabu ya Yanga ilikuwa na points (0.5) CAF, baada ya misimu (2) wamekusanya points (31). Yanga wanazidi kupanda kwa kasi.
Simba akiingia robo fainali points zitakuwa hivi; Yanga SC atakuwa amekusanya alama 31 kwa miaka miwili wakati Simba atakuwa amekusanya alama 39 kwa miaka mitano.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment