Mashabiki wa Soka wa Klabu ya Wydad Athletic Club ya Morocco, wameipigia magoti Asec Mimosas, kwa kuitaka ihakikishe inaifunga Simba SC katika mchezo wa leo Ijumaa (Februari 23).
Itazame mechi ya Asec vs Simba Live kwenye app yetu bure bofya hapa KUIDOWNLOAD
Asec Mimosas leo Ijumaa itakuwa mwenyeji wa Simba SC katika mchezo wa Mzunguuko watano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, utakaopigwa katika Uwanja wa Felix Houphouet Bounie, mjini Abidjan-Ivory Coast.
Mshabiki wa Wydad Athletic Club wamewasilisha ombi hilo kwa Asec Mimosas kupitia kurasa zao wa Mitandao ya Kijamii, wakiitaka klabu hiyo kufanya kama mataifa yao yalivyofanya kwenye ‘AFCON 2023’.
Mshabiki hao wanaamini Morocco waliisaidia Ivory Coast kuendelea katika Michuano ya ‘AFCON 2023’ kufuatia sare walioipata dhidi ya DR Congo, huku wenyeji hao wakipita kama ‘Best Looser’.
“Tuliisaidia nchi yenu kufuzu hatua ya mtoano na baadae kushinda taji la AFCON 2023, ni wakati wenu sasa kurudisha fadhila kwa klabu yetu,” wameandika mashabiki wa Wydad Athletic Club.
USikose kuitazama mechi hii live bure kwenye app yetu bofya hapa kuidownload app
Endapo Simba SC itapoteza mchezo wa leo dhidi ya Asec Mimosas na Wydad Athletic Club ikachomoza na ushindi dhidi ya Jwaneng Galaxy kesho Jumamosi, Klabu hiyo ya Morocco itakuwa imefufua matumaini ya kutinga hatua ya Robo Fainali, huku ikisubiri hatma yake katika mchezo wa Mzunguuko wa mwisho wa Kundi B.
Kama ikitokea Simba SC inashinda mchezo huo ama kutoa sare dhidi ya Asec Mimosas, Wydad Athletic Club itaendelea kuwa katika nafasi ngumu ya kupenya kutoka hatua ya Makundi kuelekea hatua ya Robo Fainali.
Post a Comment