Marcos Paquetá, Kocha Mkuu wa CR Belouizad juzi amejikuta akitaka kuzichapa na mchezaji wake aliyekuwa benchi baada ya kipigo cha bao 4-0 kutoka kwa timu ya Wananchi, Yanga SC.
Katika mchezo huo wa raundi ya tano wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika Dimba la Mkapa, Belouizad walikubali kichapo hicho na kuondoshwa kwenye michuano hiyo huku Yanga akifanikiwa kusonga mbele hatua ya robo fainali.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Mudathir Yahyadakika ya 43, Aziz Ki dakika ya 46, Kennedy Musonda dakika ya 48 na msumari wa mwisho ukishindiliwa na straika mpya, Gnadou Joseph Guede 84.
Baada ya kipigo hicho, Kocha Paquetá alimyanyua mchezaji wake kwa ajili ya kwenda kujaribu kufanya lolote kuokoa jazi hilo ambalo lilikuwa ninazama, lakini mchezaji huyo aligoma kunyanyuka kuingia uwanjani jambo ambalo kocha huyo alikasirika na kuchukua chupa ya maji akitaka kumpiga nayo
Hata hivyo, maofisa wa CAF na baadhi ya viongozi wa Belouizad walimtuliza kocha huyo raia wa Brazil aliyekuwa amepandwa na midadi ambaye hata baada ya mchezo hakuzungumzia nini kilitokea na wamemalizaje ugomvi wao.
No comments:
Post a Comment