Yanga kuwasilisha malalamiko yao Jeshi la Polisi leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuwasilisha malalamiko yao Jeshi la Polisi leo

 Yanga kuwasilisha malalamiko yao Jeshi la Polisi leo

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga amesema leo klabu hiyo itawasilisha rasmi malalamiko yake kwenye mamlaka juu ya kitendo cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga jana kwa Mkapa.


"Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisa, hakuna sababu ya msingi kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni Watani wa jadi sio maadui"


"Isije kufika siku hatuwezi kukaa kwa pamoja kama ndugu kwa sababu ya UPUMBAVU kama huu. Naiomba Bodi ya Ligi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Jeshi la Polisi ili wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe.


"Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama.. Shame on you all who're involved in this incident.


"Mwenye kumjua na kuwa na mawasiliano ya huyu (Shabiki wa Yanga aliyepigwa na mashabiki wa Simba) anitumie tafadhali" amesema wakili Simon Patrick.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz