Yanga kuongeza mshambuliaji kabla ya hatua ya makundi CAF CL - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuongeza mshambuliaji kabla ya hatua ya makundi CAF CL


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kabla ya kuanza kwa mechi za hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL), dirisha la usajili la CAF linatarajiwa kufunguliwa kwa timu ambazo katika awamu ya kwanza ya usajili hazikutimiza wachezaji 40


Hii inaweza kuwa nafasi nyingine kwa Yanga kuimarisha kikosi zaidi kwa ajili ya mikiki mikiki ya kuanzia hatua ya makundi kwani katika awamu ya kwanza ya usajili Yanga iliandikisha wachezaji 29


Katika moja ya mahojiano yake baada ya mchezo dhidi ya Al Merrikh ambao Yanga ilikata tiketi ya kutinga makundi, Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi alidokeza uhitaji wa maboresho kwenye maeneo machache


"Tunakwenda kushindana kwenye hatua ya makundi. Ili tuwe washindani bora zaidi ni wazi tutahitaji maboresho katika maeneo machache, hilo liko ndani ya mipango ya uongozi lakini kama kocha, wakati wote unahitaji zaidi"


"Pasipo na shaka, tunahitaji maboresho kidogo ili tuwe washindani bora zaidi dhidi ya timu kubwa," alisema Gamondi


Eneo ambalo Gamondi alilenga ni wazi ni katika safu ya ushambuliaji ambapo bado usajili wa Mghana Hafiz Konkoni 'haujawaka'


Katika mechi za karibuni Gamondi amewatumia zaidi Clement Mzize na Kennedy Musonda wakati Konkoni akipata dakika chache kwenye baadhi ya mechiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz