Ronaldo apewa adhabu ya kuchapwa viboko 99 - EDUSPORTSTZ

Latest

Ronaldo apewa adhabu ya kuchapwa viboko 99

 Ronaldo

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Siku ya leo Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kuwa Mshambuliaji wa klabu ya Alnassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amepewa hukumu ya kuchapwa viboko 99 kwa kosa la uzinzi pindi ambapo atakakanyaga nchini Iran kwa mujibu wa sheria za Kiislam.


Hii ilitokea wakati Al Nassr wamepewa mapokezi ya nguvu nchini Iran wakati Al Nassr ilipocheza na Persepolis katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya huko barani Asia katika mji mkuu wa Iran Tehran.


Tukio lilikuwa hivi: Wakati Ronaldo anakaribishwa nchini humo, alipewa zawadi kutoka kwa mashabiki wanaompenda, ikiwa ni pamoja na picha zilizochwa sura yake kutoka kwa msanii Fateme Hamami ambaye ni mwanamke.


Katika kumshukuru Hamami kwa zawadi yake hiyo, Ronaldo alikumbatiana mchoraji huyo na kumbusu shavuni, jambo ambalo liliwakasirisha kundi la wanasheria wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iran kwa sababu chini ya sheria za Iran, kumgusa mwanamke ambaye sio mke, Dada au mama yako au ndugu yako yoyote wa karibu ni uzinzi na kuna adhabu zako.


Mojawapo ya adhabu hizo ni kuchapwa viboko 99.


Kupitia Iran Sharq Emroz imeelza kuwa tayari hukumu imeshatolewa kwa Ronaldo na atachapwa viboko 99 kwa kosa la uzinzi wakati mwingine atakapoingia nchini Iran.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz