Ahmed Ally awaomba jambo hili mashabiki wa Simba kuelekea mechi Yao dhidi ya Al Ahly - EDUSPORTSTZ

Latest

Ahmed Ally awaomba jambo hili mashabiki wa Simba kuelekea mechi Yao dhidi ya Al Ahly

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema haijawahi kuwa jambo gumu kwa Simba kupata ushindi dhidi ya Al Ahly katika mechi zinazopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa


Ahmed amesema safari hi kwenye michuano ya African Football League, Simba imedhamiria sio kushinda tu kwenye uwanja wa Mkapa bali ni kuwaondosha kabisa mashindanoni mabingwa hao wa Afrika


Akizungumza mapema jana Buguruni katika droo ya makundi ya mechi za matawi ambayo yatashiriki AFL Simba Beach Bonanza, Ahmed aliwataka Wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa Ijumaa ijayo ili kuwaongezea hamasa wachezaji wao na kuhakikisha wanapata ushindi mnono dhidi ya Al Ahly


Pamoja na kufahamu ugumu wa mchezo huo, Ahmed amesema umoja na ushirikiano wa Wanasimba wote utakuwa silaha muhimu katika kuhakikisha wanatimiza malengo yao


"Kwenye mechi ya tarehe 20 tunahitaji ushirikiano wa kila Mwanasimba. Lazima tuambiane ukweli Al Ahly ni mpinzani mgumu, bila kujikaza tutapata tabu lakini tukiwa pamoja hata wakija wote na farao tutawafunga Kwa Mkapa nyingi"


"Ni lazima tupambane ili tukamfunge. Simba kumfunga Al Ahly sio jambo kubwa hata wao wanajua hilo sio jambo ngumu lakini safari hii kuna kazi maalumu ya kumtoa kwenye mashindano hilo ndio jambo hatujawahi kufanya, hilo ndio tunatafuta"


"Tunawaheshimu ni timu kubwa Afrika lakini hata Daudi angemuogopa Goliati asingempiga. Na udogo wake Daudi lakini alimuangusha Goliati na ukubwa wake. Simba ndio kitu tunakwenda kufanya tarehe 20"


"Dhamira ya kumuangusha Al Ahly itatimizwa na kila Mwanasimba. Ili jambo letu liweze kutimia lazima sisi kama mashabiki tutimize jukumu letu la kwenda uwanjani"


"Haya ni mashindano mapya duniani, mara ya kwanza Afrika na zimechaguliwa timu nane zinazojua tu. Watu wengi wanatamani wangepata hii nafasi, wanawaonea gere kwelikweli, sio wao tu, watu wote wa Afrika Mashariki na Kati kwa nafasi tuliyonayo"


"Katika kipindi tunatakiwa kuringa na timu yetu basi ni hiki. Walikaa watu wa CAF wakaona Simba pekee ndio inastahili kutoka Tanzania inastahili kushiriki African Footbal League. Inawakera wengine vibaya sana, inawauma sana," alitamba AhmedDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz