Ratiba: Simba itaanzia kwa Mkapa na kumalizia kwa Mkapa makundi CAF - EDUSPORTSTZ

Latest

Ratiba: Simba itaanzia kwa Mkapa na kumalizia kwa Mkapa makundi CAF

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Jana Wanamsimbazi walifahamu kundi ambalo Simba imepangwa katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika


Simba iliyojiwekea malengo ya kucheza nusu fainali katika msimu huu, imepangwa kundi B pamoja na Jwaneng Galaxy, Asec Mimosas na Wydad Athletic


Habari njema zaidi kwa Simba ni kuwa mechi ya kwanza katika hatua ya makundi watacheza nyumbani na pia mechi ya mwisho watamaliza nyumbani


Asec Mimosas watakuwa wa kwanza kuvuta pumzi ya moto katika uwanja wa Benjamin Mkapa, mchezo ukitarajiwa kupigwa Novemba 24-26 2023


Baada ya mchezo huo Simba itasafiri Botswana kuikabili Jwaneng Galaxy Disemba 01-02 kisha kuelekea Morocco kuikabili Wydad Athletic Disemba 08-09


Disemba 19 Wydad atakuja Tanzania kuvuta pumzi ya moto kabla ya Simba kusafiri Ivory Coast kuikabili Asec Mimosas February 23-24


Hesabu za makundi zitafungwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa March 01-02 kwa mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy


Hii inaweza kuwa mechi ya kuipeleka Simba robo fainali na hakuna shaka itakuwa mechi ya kisasi pia kwa hawa 'Makiri-kiri'Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz