Kocha Stars awatema Fei Toto, Kapombe na Tshabalala - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Stars awatema Fei Toto, Kapombe na Tshabalala

 Kocha Stars awatema Fei Toto, Kapombe na Tshabalala

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche ameendelea kuwapotezea kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' na mabeki wa Simba wa pembeni Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Shomari Kapombe.


Katika orodha ya wachezaji 28 wa Stars inayokwenda kucheza dhidi ya Sudan kwenye mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya Shirikisho la Soka Dunaini (FIFA) Amrouche pia amemtema kiungo wa Yanga Jonas Mkude.


Orodha hiyo imewajumuisha makipa Beno Kakolanya (Singida Big Stars), Metacha Mnata (Yanga), Ally Salim (Simba).


Mabeki ni Israel Mwenda(Simba),Abdulrazak Hamza(Super Sport United), Nickson Kibabage, Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job (wote Yanga), Abdi Banda( Richards Bay),Haji Mnoga (Aldershot Town)


Viungo waliojumuishwa ni Kibu Denis, Mzamiru Yassin (wote Simba),Mudathir Yahya (Yanga), Abdul Seleman (Azam), Baraka Majogoro (Chippa United), Abdulmalik Zakaria (Namungo), , Sospeter Bajana(Azam), Himid Mao (Tala'ea El Gaish), Ben Starkie (Basford United), Morrice Abraham (FK Sportak Subotica).


Washambuliaji ni Mbwana Samatta( Paok FC), Simon Msuva ( JS Kabylie), Clement Mzize (Yanga), Said Khamis (FK Jedinstvo), George Mpole (FC Lupopo) na Nassoro Saadun (Ihefu).


Starsa itaondoka nchini kesho ikielekea Saudi Arabia itakapocheza dhidi ya Sudan, mchezo utakaofanyika Oktoba 15.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz