Alicho kisema Kocha mkuu wa yanga kuelekea mechi ya Kesho - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kisema Kocha mkuu wa yanga kuelekea mechi ya Kesho


Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema licha ya changamoto ya ratiba, kikosi chake kitakuwa tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi amesema ratiba sio rafiki kwa sababu hakuna muda wa kufanya mazoezi hata hivyo kama kocha anafahamu  ziko nyakati ratiba inaweza kuwa ngumu wanapaswa kuwa tayari kucheza wakati wowote


"Maandalizi kwa upande wetu siyo mazuri sana kutokana na ratiba lakini sisi ni wataalamu na ligi kuna muda inakuwa na ratiba ngumu lazima kuwa tayari. Leo tutakuwa na mazoezi jioni, ambayo yatatusaidia kuona hali ya wachezaji kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold"


"Nafahamu kesho tutakuwa na mchezo mgumu na sijui hali ya Uwanja ikoje lakini nafikiri itakuwa kama Uwanja wa mchezo wetu uliopita. Ukweli nina wasiwasi sana na viwanja pamoja na maamuzi ya waamuzi uwanjani nina imani kutakuwa na mabadiliko kwenye hili kwasababu kila kitu kinaonekana wazi"


"Tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu, lakini mashabiki wameendelea kuwa pamoja nasi na kutupa sapoti kama vile bado hatujapoteza mchezo wowote ni kazi yetu sasa kuhakikisha kwenye mchezo wa kesho tunajitoa kwa nguvu zote kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Gamondi


Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc juzi kwa kufungwa  mabao 2-1, ni wazi Gamondi na vijana wake wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Geita GoldDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz