Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mpaka sasa, Yanga imethibitisha kuwa mabasi saba yamejaa baada ya mashabiki na Wanachama kulipia gharama ya safari
Kutakuwa na mabasi maalum kutoka jijini Dar es salaam ambayo gharama ni Tsh 150,000/- kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na tiketi ya kuingia dimba la Pele, Kigali Jumamosi Septemba 16 2023
Pia kutakuwa na mabasi kutoka mikoa ya Kigoma, Kagera na Mwanza ambapo utaratibu unaandaliwa katika Matawi ya mikoa husika
Uwanja wa Pele unachukua takribani mashabiki 22,000, Wananchi wamepania kwenda kuujaza uwanja huo
Hapo bado hujazungumzia Wananchi wa Rwanda ambao wanaisubiri kwa hamu kubwa Yanga
Safari itakuwa Alhamisi Septemba 14, bado mashabiki wanaendelea kujitokeza ambapo zoezi litafungwa Jumanne ijayo, Septemba 12
Kwa hakika huko Rwanda Yanga itakuwa kama nyumbani tu
No comments:
Post a Comment