Mahakama yaamuru Bocco alipwe Tsh Milioni 200 - EDUSPORTSTZ

Latest

Mahakama yaamuru Bocco alipwe Tsh Milioni 200

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mahakama Kuu ya Tanzania, imeiamuru kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Princes Leisure (T) Ltd ya jijini Dar es Salaam, kumlipa mchezaji wa Simba, John Raphael Bocco, Sh200 milioni kwa kutumia picha yake katika tangazo la Biashara


Hukumu hiyo ilitolewa wiki iliyopita Agosti 31, 2023 na Jaji Irvin Mugeta wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam


Awali Bocco aliiomba mahakama iiamuru kampuni hiyo kumlipa Sh1 bilioni kama fidia, kutamka kuwa ilitumia picha yake bila kuwa na mamlaka nayo na kumlipa mrabaha wa asilimia 25 kipindi chote ilichoitumia


Tangazo hilo likiwa na picha ya Boko lililotolewa katika ukurasa wa Instagram wa kampuni hiyo kati ya Novemba 18, 2021 hadi Desemba 1, 2021 na ujumbe huo ulisomeka katika mtandao huo wa kijamii ukisema;


"Uhondo wa Ligi NBC unaendelea leo kwa mechi 3. Kubwa zaidi ni Simba watakuwa wageni wa Ruvu Shooting huko Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba. Siku za Pesa zimerejea,” na kusambaa ndani na nje ya Tanzania.


Bocco katika kesi hiyo aliyowakilishwa na mawakili Innocent Michael na Gadi Kabele, alisema kutumiwa kwa picha yake kulimaanisha amevunja mkataba wake na Simba na timu hiyo ilikuwa iko mbioni kumchukulia hatua za kinidhamu


Kesi hiyo namba 118 ya mwaka 2022 ilisikilizwa upande mmoja (ex parte) kwa kuwa mdaiwa aliondolewa katika mwenendo wa shauri hilo baada ya kushindwa kuwasilisha utetezi wake kwa maandishi kwa muda ulio ndani ya sheria


Kesi hiyo ilisikilizwa na Jaji Mugeta Agosti 25, 2023 na hukumu ikatolewa Agosti 31 na nakala ya hukumu hiyo kuwekwa katika mtandao wa mahakama (Tanzill) mahsusi kwa ajili ya kuchapisha maamuzi, sheria na kanuni bure mtandaoni


MwanaspotiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz