Waliokuwa timu za taifa kuripoti kambini Jumatatu - EDUSPORTSTZ

Latest

Waliokuwa timu za taifa kuripoti kambini Jumatatu

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Baada timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kurejea nchini kutoka Algeria ambako walifanikiwa kufuzu michuano ya Afcon 2023, nyota wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi hicho wanatarajiwa kurejea kambini kesho Jumatatu kuendelea na maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa


Jumamosi ijayo, Septemba 16 Yanga itakuwa Rwanda kuchuana na AL Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Miguel Gamondi alitoa mapumziko kwa siku ya leo Jumapili


Aidha Kamwe amesema Yanga inafanya utaratibu wa kumsafiri kiungo Stephane Aziz Ki ambaye yuko Morocco na timu ya Taifa ya Burkina Faso


"Kocha (Gamondi) alitoa mapumziko kwa wachezaji wote siku ya leo hivyo tunatarajiwa hapo kesho wote ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa katika majukumu ya timu ya Taifa wataripoti mazoezini"


"Kuhusu kiungo wetu Stephane Aziz Ki ambaye yuko Morocco ambako walipaswa kucheza dhidi ya Morocco lakini mchezo huo umeahirishwa kutokana na tetemeko la arhi lililokumba nchi hiyo"


"Tumewasiliana nae, yuko salama na wachezaji wenzake wa Burkina Faso, uongozi umewasiliana na FA ya Burkina Faso na tunaandaa utaratibu kuhakikisha Aziz Ki anarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Merrikh," alisema KamweDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz