Man United wachezea kichapo mbele ya Arsenal - EDUSPORTSTZ

Latest

Man United wachezea kichapo mbele ya Arsenal

Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao 3-1

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Wenyeji, Arsenal wametoka nyuma na kuwaadhibu Manchester United kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumapili Uwanja wa Emirates Jijini London.


Man United ilitangulia na bao la Marcus Rashford dakika ya 27, kabla ya Arsenal kuzinduka kwa mabao ya Martin Ødegaard dakika ya 28, Declan Rice dakika ya sita ya muda wa ziada na Gabriel Jesus dakika ya 11 ya muda wa ziada baada ya kukamilika dakika 90 za kawaida za mchezo.


Kwa ushindi huo, Arsenal wanafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya tano, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao sita na kushukia nafasi ya 11 baada ya wote kuchezea mechi nne.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz