Kocha mkuu wa Yanga awashangaza wengi baada ya kufanya hili - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha mkuu wa Yanga awashangaza wengi baada ya kufanya hili

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesisitiza kuwa katika kikosi chake anataka kuona kila mchezaji anaweza kufunga mabao pale anapopata nafasi


Katika misimu miwili iliyopita, Yanga ilimtegemea zaidi mshambuliaji Fiston Mayele ambaye ametimkia Pyramids Fc ya Misri


Wakati Mayele anaondoka wengi waliamini Yanga itayumba kwa sababu Mcongomani huyo alichangia karibu asilimia 80 ya mabao yaliyofungwa na Yanga


Hata hivyo tangu ujio wa Gamondi ni kama falsafa ya timu hiyo katika ushambuliaji imebadilika wafungaji wakiwa wengi


Gamondi ameeleza sababu kwa nini hapendi timu yake iwe tegemezi kwa mchezaji mmoja katika kufunga mabao


"Ikiwa utakuwa unawategemea washambuliaji peke yake inakuwa rahisi kwa wapinzani kuwapa presha hao wachezaji na mwisho watakwama kukupa ushindi"


"Kila mchezaji anafunga awe ni beki, kiungo na hata washambuliaji nao wanafunga jambo ambalo ni zuri kwetu. Makosa yanayojitokeza tunaendelea kuyarekebisha lakini jambo muhimu kwetu kwa kiasi kikubwa tumeweza kukamilisha malengo yetu katika mechi zilizopita," amesema Gamondi


Katika orodha ya wafungaji ligi kuu ya NBC, washambuliaji Hafiz Konkoni na Kennedy Musonda kila mmoja amefunga bao moja wakati viungo Stephane Aziz Ki, Mudathir Yahya na Max Nzengeli kila mmoja amepachika mabao mawili


Wachezaji wengine waliofunga mabao ni Yao Kouassi, Pacome Zouzoua na Dickson JobDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz