Kocha Al Merrikh aichimba Yanga mkwara "Tutacheza kama Fainali" - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Al Merrikh aichimba Yanga mkwara "Tutacheza kama Fainali"

 Kocha Mkuu wa Al Merrikh, Osama Nabih

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Wakati Al Merrikh wakijiandaa kuivaa Yanga mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu kwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kocha Mkuu wa Kikosi cha Al Merrikh Osama Nabih amesema wanakwenda kucheza mchezo huo kwa juhudi zote kwani wapinzani wao Yanga sio timu ya kuchezea hata kidogo.


Akizungumza Nabih anasema;


“Wenzetu (Yanga) ukiangalia mechi zao wanaonekana wako tayari. Ni timu ambayo iko fiti na kitu kibaya zaidi kwetu ni kwamba wameshinda mechi za ligi kwa idadi kubwa ya magoli na mbili zaKlabu Bingwa Afrika” alisema Nabih


“Tunalazimika kucheza mechi kama hizi za kirafiki ambazo sawa zinaweza kutusaidia, lakini sio kwa ukubwa kama utakapocheza mechi za ushindani kama ligi. Tutaendelea kujipanga zaidi tukiangalia kama tutapata mechi nyingine hapa karibuni ya kirafiki.“


“Ubora wao mkubwa uko eneo la kiungo mechi ambazo tumeziangalia kama hatutakuwa na ubora wa kuwadhibiti eneo hilo tunaweza kufanya makosa, lakini pia kwenye ulinzi pia ni timu nzuri.


“Haitakuwa mechi rahisi kwetu na hata kwao, nimewaambia wachezaji wangu hii ni sawasawa na Fainali kwetu itakayoamua safari yetu kwenye mashindano haya, tunatakiwa kucheza kama wanajeshi.”


Yanga watacheza na Al Merrikh nchini Rwanda Septemba 16 mchezo wa Mkondo wa kwanzaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz