Gamondi achimba mkwara licha ya Yanga kushindwa 2-0 Rwanda - EDUSPORTSTZ

Latest

Gamondi achimba mkwara licha ya Yanga kushindwa 2-0 Rwanda

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Pamoja na kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Al Merrikh, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema bado hawajakata titeki ya kutinga hatua ya makundi na watahitaji kujiandaa vyema ili kuhakikisha wanashinda mechi ya marudiano itakayopigwa Septemba 30 katika uwanja wa Azam Complex


Aidha Gamondi amesema kwa sasa wanaweka nguvu katika mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumatano, baadae watarejea Avic Town kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Merrikh ambao ndio utaamua hatma yao kuelekea hatua ya makundi


Hata hivyo Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Pele Kigali, Rwanda na Yanga kushinda mabao 2-0


"Tulikuwa na dakika 90 nzuri, nawapongeza sana wachezaji wangu, licha ya ugumu wa mchezo hasa kipindi cha kwanza, ila walirudi kipindi cha pili na akili kubwa ya kutafuta ushindi na tukafanikiwa"


"Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini nadhani tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu kulingana na jinsi tulivyotengeneza nafasi za wazi"


"Mechi ya kwanza imekwisha, sasa tunatakiwa kuhamisha akili kwenye mechi ya ligi na baada ya hapo tutamalizana na wapinzani wetu hao wa CAF, nataka nikwambie bado hatujafuzu, ushindi mzuri unatakiwa kuwa mechi hii ya pili, hata wao wanaweza kutufunga kwetu kama hatutakuwa makini," alisema Gamondi ambaye alirejea nchini jana na kikosi cha YangaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz