Al Ahly wapigwa 'stop' kutumia simu mpaka wamalizane na Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Al Ahly wapigwa 'stop' kutumia simu mpaka wamalizane na Simba

 Al Ahly wapigwa 'stop' kutumia simu mpaka wamalizane na Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha Marcel Koller amewataarifu wachezaji wake wa Al Ahly kuwa wamefungiwa kutumia mitandao ya kijamii hadi angalau mwisho wa mchezo wao wa Ligi ya Soka dhidi ya Simba SC.

Ametaja Sababu ni kwamba, kocha huyo anahisi kuna hali ya uzembe miongoni mwa wachezaji kabla ya mechi muhimu hivyo ameamua hakuna kuchapisha picha wala video kwenye mitandao.

Wiki iliyopita Ahly wametoka kuchezea kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa CAF Super Cup na kupoteza kombe hilo baada ya kufungwa na USM Alger ya Algeria, mchezo uliopigwa nchini Saudi Arabia.

Septemba 24, Ahly itacheza mchezo wa raundi ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi St. George ya Ethiopia kabla ya kurudiana Septemba 29, 2023.

Oktoba 20, 2023, Ahly watacheza na Simba SC kwenye mchezo wa African Football League kwenye mechi ya ufunguzi katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz