Wafahamu wapinzani wa Yanga ASAS FC klabu bingwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Wafahamu wapinzani wa Yanga ASAS FC klabu bingwa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Association Sportive d'Ali Sabieh Djibouti Telecom (ASAS Fc)  ni klabu kutoka Djibouti, wanashiriki kwenye ligi kuu ya Djibouti


Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1991, inamiliki uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Aptidon, wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000.


ASAS FC wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Djibout mara saba na Djibouti Cup mara tatu ndio klabu iliyofanikiwa zaidi nchini humo


Hawajawahi kuvuka hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa wala kombe la Shirikisho barani Afrika


Msimu uliopita ilishiriki kombe la Shirikisho ikatupwa nje hatua ya awali kwa kufungwa bao 1-0 na AS Kigali ya Rwanda


Jumapili ya wiki hii watakuwa Tanzania kuchuana na Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika


Kwa kuwa uwanja wao haukukidhi vigezo vya CAF, timu hiyo imelazimika kucheza mechi yake ya nyumbani katika uwanja wa Azam Complex


Mchezo wa kwanza ukipigwa August 20 wakiwa wenyewe na mchezo wa pili utapigwa August 28 Yanga wakiwa wenyeji


Mechi zote mbili kupigwa Tanzania ni faida kubwa kwa Yanga, vijana wa kocha Miguel Gamondi wana kazi ya kuhakikisha wanamaliza mechi Jumapili ili mchezo wa marudiano uwe wa kukamilisha ratiba tuDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz