Viingilio Yanga vs Asas Fc CAF Confederation cup - EDUSPORTSTZ

Latest

Viingilio Yanga vs Asas Fc CAF Confederation cup

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex siku ya Jumamosi, August 26 katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Asas Fc


Kamwe amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujihakikishia tiketi ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ikiwa ni hatua moja kuelekea makundi


"Mchezo huu haujamalizika kama wengi wanavyosema. Unapodharau mpinzani kwa sekunde moja tu, mechi inaweza kubadilika. Iko mifano mingi tu, kuna timu ziliwahi kushinda ugenini na kupoteza nyumbani"


"Kwa kuwa tuna dakika 90 za kucheza hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu. Tunaomba mashabiki wetu mje kwa wingi kushangilia ili kuhakikisha tunasonga mbele. Nawaomba mashabiki tusiingie katika mtego wa kudhani mechi imemalizika"


Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo ambapo Mzunguuko ni Tsh 5,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na VIP A ni Tsh 30,000/-


Kamwe amewaasa mashabiki kuhakikisha wananunua tiketi zao mapema, wasisubiri kukata tiketi uwanjani kwani kuna matukio ya kuuziwa tiketi feki


Aidha Kamwe amesema siku hiyo imepewa jina la 'Max Day', Wananchi wataitumia kumuenzi mchezaji wao Max Nzengeli kwa kuchomekea


"Kwa yeyote atakayekuja uwanjani ahakikishe amechomekea, huu ndio utakuwa mtoko wetu wa Max Day," alisema KamweDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz