Mcheza mieleka Bray Wyatt afariki dunia, WWE yathibitisha - EDUSPORTSTZ

Latest

Mcheza mieleka Bray Wyatt afariki dunia, WWE yathibitisha

Mcheza mieleka Bray Wyatt afariki dunia, WWE yathibitisha

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mcheza mieleka maarufu duniani, Bray Wyatt amefariki dunia jana Agosti 24, 2023 akiwa na umri wa miaka 36. Kifo chake kimethibitishwa na chama cha mieleka dunia (WWE) huku sababu za kifo cha staa huyo hazikutajwa.


Wyatt, ambaye jina lake halisi ni Windham Rotunda, alikuwa mtoto wa mwanamieleka wa WWE Hall of Fame, Mike Rotunda.


"Mawazo yetu yapo kwa familia yake na tunaomba kila mtu aheshimu faragha yake kwa wakati huu," Paul "Triple H" Levesque, Ofisa mkuu wa maudhui wa WWE, alisema kwenye mtandao wa kijamii.


Wyatt alikua Bingwa wa WWE mnamo 2017 na alishindana kama wahusika wengi wakati wa kazi yake, pamoja na kama mshiriki wa Familia ya Wyatt na kama mtu aliyejificha kwa jinamizi aitwaye Fiend.


Mwanamieleka huyo alikuwa akiunda kundi la watu watatu lililopewa jina la The Wyatt Family likiwa na majina kama, Erick Rowan, Luke Harper nay eye mwenyewe.


Chanzo: MwanaspotiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz