Simba waondolewa kwenye Ligi Kuu Oktoba hadi Novemba - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba waondolewa kwenye Ligi Kuu Oktoba hadi Novemba


Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo amesema waandaaji wa mashindano ya Super League wameomba klabu ya Simba itolewe kwenye ratiba ya Ligi Kuu Bara kuanzia Oktoba 20 hadi Novemba 21 kwa ajili mashindano ya kimataifa ya African Super League.


Almasi aliyasema hayo jana Agosti 7, 2023 alipokuwa akitangaza ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023-24.


"Wameomba na ndio maana unaona michezo yao katika kipindi hicho tumeiwekea TBA, hivyo michezo yao watakuja kuicheza pale nafasi itakapopatikana," alisema Kasongo.


Hivyo Simba, watasimama kwa takriban mwezi mzima kwenye Ligi Kuu isipokuwa mchezo mmoja wa dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga (Novemba 5) ambao kwa mujibu wa Kasongo, umeachwa tarehe hiyo mpaka pale Shirikisho la Mpira Afrika watakaposema vinginevyo.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz