Alicho kisema Ghalib Said Mohamed ( GSM ) kuhusu Documentary Ya Yanga hapo jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kisema Ghalib Said Mohamed ( GSM ) kuhusu Documentary Ya Yanga hapo jana

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Sasa ukiacha na mafanikio yao hauwezi kuacha kumtaja muwekezaji namba moja GSM yaani mdhamini Mkuu na kupitia documentary yao wamempa nyota tano mabegani ikiwa kama ishara ya kumpa pongezi kwa kuendelea kuwa mdhamini mkuu katika klabu hiyo.


Aidha Ghalib Said Mohamed aliweza kuzungumza machache na vyombo vya habari baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa documentary hiyo na kusema…’Ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza Young Africans kwa mafanikio Mwaka 2022/23 kwa kuchukua ubingwa wa Ngao ya Jamii, Ubingwa wa Ligi Kuu, Ubingwa Azam Sports Federation CUP na kufika fainali ya CAF hakika haya ni mafanikio makubwa ya Club yetu’


‘Sasa hivi wanaelekea kuanzia msimu 2023/24 naamini Yanga Bingwa tena rekodi inaenda kuandika kama mlivyoshuhudia kile kilichopo kwenye Documentary ili vizazi na vizazi waje kujua mengi kuhusu Young Africans basi hivyo hivyo tunaenda kuiandika rekodi nyingine katika msimu huu mpya na inshallah Mwenyezi Mungu atupe umri na Afya tele tukutane hapa hapa kushuhudia Documentary ya msimu wa 2023/24 Yanga Bingwa’- Mkurugenzi na Rais wa GSM, Ghalib Said MohamedDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz