Pluijm alia na mwamuzi mechi dhidi ya Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Pluijm alia na mwamuzi mechi dhidi ya Simba

 

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha Mkuu wa Singida FG Hans van Pluijm amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba


Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jana ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana


Hata hivyo Pluijm amesema walistahili kupata zaidi ya walichokipata huku akimtupia lawama mwamuzi Amina Kyando


"Nawapongeza wachezaji wangu tulikuwa na mchezo mzuri leo. Siwezi kuwalaumu kwa kupoteza kwenye penati. Tulicheza vizuri hasa kwenye kipindi cha kwanza, tulifunga goli ambalo kwa maoni yangu lilikuwa halali sijajua kwa nini mwamuzi alikataa. Lakini pia dakika za mwisho tulipata nafasi nzuri mwamuzi akamaliza mchezo wakati mchezaji wetu akijiandaa kupiga mpira"


"Tangu mwanzo tulisema, sisi hatukuja kushirki Ngao ya Jamii tu, bali tumekuja kushindana. Tunakwenda kujiandaa kwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Azam Fc," alisema PluijmDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz