Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Winga wa Yanga Jesus Moloko amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu na sasa yuko tayari kwa mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, August 13 katika uwanja wa Mkwakwani
Adhabu hiyo aliipata msimu uliopita baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa uwanja wa Sokoine na kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 3-3
Moloko alikosa michezo dhidi ya Tanzania Prisons (Ligi Kuu) na mechi mbili dhidi ya Azam Fc kuanzia mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu uliopita na nusu fainali ya Ngao ya Jamii
Hii ni habari njema kwa Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ambaye atakuwa na machaguo mengi katika eneo la winga kuelekea mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumapili mechi itakuwa mubashara kwenye app YETU kama bado hujaipakua BOFYA HAPA
Post a Comment