Mandonga achezea kichapo tena Zanzibar - EDUSPORTSTZ

Latest

Mandonga achezea kichapo tena Zanzibar

 Mandonga apigwa tena

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Bondia Muller Jr ameibuka mshindi kwenye pambano la Raundi Sita dhidi ya Karim Mandonga pambano la Tamasha la Uzinduzi wa Mchezo wa Ngumi Zanzibar lilopigwa katika uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar.


Muller Jr ameshinda kwa uamuzi wa Majaji na kuwa moja ya walioandika historia ya kushiriki kwenye tukio la kuurejesha tena mchezo wa Masumbwi Zanzibar baada ya miaka 60 kupita bila ya mchezo huo.


Pambano hilo la Raundi Sita limeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye alijuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya ngumi yaliyopigwa marufuku Kisiwani hapo zaidi ya mika 50 iliyopita ambapo Majaji wote watatu wamempa ushindi Kiluwa kwa pointi 55-56, 56-58 na 55-59


Hii ni mara ya tatu mfululizo Mandonga kupigwa. Julai 22 alipoteza pambano la marudiano na Mkenya Daniel Wanyonyi, na Julai 29 alipoteza pambano dhidi ya mganda Moses Golola na sasa Mandonga anasema anajipanga kwa ajili ya pambano jingine.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz