Kikosi Bora kilichosajiliwa Msimu huu 2023/24 - EDUSPORTSTZ

Latest

Kikosi Bora kilichosajiliwa Msimu huu 2023/24

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Usajili wa wachezaji kwa klabu za Tanzania umeendelea kuwa gumzo kwa wiki kadhaa sasa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.


Hata hivyo, ni klabu tatu za Simba, Yanga na Azam ambazo zimekuwa zikitangaza rasmi wachezaji wao pale wanapokuwa tayari wamekamilisha taratibu huku zingine bado zikiendelea kusuasua.


Kabla hata ligi haijaanza, tayari kuna wachezaji wapya wageni waliosajiliwa wameshaanza kutabiriwa kuiteka Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mara nyingi kila msimu kumekuwa na maingizo mapya ya wachezaji wa kigeni ambao pamoja na wengine hawafanyi vizuri, lakini baadhi wanauwasha moto na kuwa vipenzi vya mashabiki wa soka kama ilivyokuwa msimu uliopita kwa Stephane Aziz Ki wa Yanga, James Akaminko wa Azam, Bruno Gomes wa Singida United na Jean Baleke wa Simba ambaye alisajiliwa kwenye dirisha dogo na haikuchukua muda kuingia kwenye vichwa vya mashabiki.


Katika makala haya, Nipashe linakuletea kikosi bora cha wachezaji 11 wapya waliosajiliwa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ambao wanatarajiwa kutikisa na kukonga nyoyo za mashabiki.


#Beno Kakolanya - Singida Fountain Gate


Pamoja na kwamba bado Singida Fountain Gate hawajamtangaza rasmi, lakini taarifa zinaeleza kipa Beko Kakolanya amesaini na klabu hiyo na ni mmoja wa wachezaji watakaowekwa hadharani kwenye Tamasha la Singida Big Day.


Kakolanya anatarajiwa kuwa mmoja wa makipa watakaotikisa ligi msimu ujao na hapana shaka anakwenda kuwa kipa namba moja kwenye kikosi hicho.


Itakuwa hivyo kwa sababu anatoka kwenye klabu kubwa ambayo imecheza mechi mbalimbali za kimataifa na yeye akiwamo, hivyo uzoefu wake utaibeba Singida Fountain Gate katika michuano mbalimbali itakayoshiriki. 


#Kouassi Attohoula Yao - Yanga


Ameonekana kwenye mechi moja tu siku ya Tamasha la Siku ya Mwananchi ambapo timu ya Yanga ilicheza dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.


Yao, aliyesajiliwa msimu huu kutoka Asec Mimosas ni raia wa Ivory Coast, pamoja na kwamba aliingia kipindi cha pili, lakini shughuli aliyoifanya ilikuwa ni ishara tosha kuwa patachimbika Ligi Kuu Tanzania Bara itakapoanza.


Ndiye aliyekuja kuchukua nafasi ya Djuma Shaaban anayetajwa kuwa anakwenda kujiunga na TP Mazembe.


#Cheikh Sidibe - Azam FC


Ni mchezaji mpya raia wa Mali ambaye mashabiki wa Bongo wataanza kumuona akiwa amevalia jezi ya Azam FC msimu wa 2023/24.


Amesajiliwa kutoka Klabu ya Teungueth ya Senegal na anacheza nafasi ya beki wa kushoto, akiwa anaonekana kuja kuchukua nafasi ya aliyekuwa nahodha wa timu hiyo na kupewa 'thank you' kuelekea msimu ujao, Bruce Kangwa.


Katika mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan iliyochezwa nchini Tunisia ambapo ipo kwa maandalizi ya msimu ujao, alipachika bao moja, Azam ikishinda 3-0, hivyo anatarajiwa kuuwasha kweli kweli kwenye Ligi Kuu Bara.


Gift Fred - Yanga


Kwa waliomuona katika mechi dhidi ya Kaizer Chiefs, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ikishinda bao 1-0, aliingia na kufanya mambo makubwa.


Hata hivyo, aina ya uchezaji wake inaonekana ni namba nne, ana nguvu, anapenda kuruka juu kuishambulia mipira mirefu iliyotumwa kwa mawinga na washambuliaji.


Akipata namba tano ambaye ametulia, kazi yake kuiokota mipira ambayo imempita, atakuwa msaada mkubwa kwa Yanga na kutishia namba za watu kwenye kikosi hicho.


Che Fondoh Malone - Simba


Ni moja kati ya sajili mpya kwenye Klabu ya Simba ambazo zitaangaliwa na macho mawili na mashabiki wengi wa soka nchini.


Beki huyo wa kati anatarajiwa kucheza pacha na raia wa Jamhuri ya Congo, Inock Inonga.


Anaweza kucheza kama namba nne na tano pia, hivyo watakuwa wanatumana. Malone aliyesajiliwa kutoka Cotonsport ya Cameroon ni raia wa nchi hiyo, ametua kuchukua nafasi ya Mkenya Joash Onyango.


Mchezaji huyu alishinda tuzo ya uchezaji bora msimu uliomalizika nchini Cameroon, kitu ambacho huwa si kawaida sana kwa mabeki, hivyo kuna kitu tofauti anaonekana atakionyesha kwenye Ligi Kuu.


Fabrice Ngoma - Simba


Ligi ya Tanzania Bara msimu huu itakuwa na mchezaji mmoja fundi aliitwaye Fabrice Ngoma. Ni mcheaji mwenye uwezo wa kucheza kiungo mkabaji, lakini msaidizi wa kiungo mkabaji maarufu kama namba nane.


Mashabiki wa soka wanataka kuona ufundi wake aliotoka nao AS Vita Club mpaka Al Hilal Omdurman ya Sudan ambako Simba imekwenda kumsajili huko.


Luis Miquissone - Simba


Mashabiki wa soka si Tanzania tu, bali Afrika nzima wanataka kuona kama winga huyu atakuwa na ubora ule ule ambao alitoka nao.


Kwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba msimu huu, mategemeo namba moja ya wanachama na mashabiki ni kwa Luis, raia wa Msumbiji kwa sababu wanaufahamu ubora wake wakati akiichezea timu hiyo msimu wa 2020/21 aliposajiliwa kutoka UD Songo alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka klabu mama ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kabla ya kuuzwa Al Ahly ya Misri 2021. Hapa anachukuliwa kama usajili mpya licha ya kwamba ameshawahi kucheza Ligi Kuu nchini huko nyuma.


Pacoma Zouzou - Yanga


Ni kiungo wa kati, namba nane ambaye Yanga ilimsajili kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast. Hakucheza kwenye mechi dhidi ya Kazer Chiefs na sababu bado hazijatajwa, lakini anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji watakaotikisa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.


Alassane Diao - Azam


Moja ya mastraika wapya wa kutazamwa kwenye Ligi ya Tanzania msimu ujao ni Alassane Diao raia wa Senegel.


Amesajiliwa na Azam FC, ikiwa na nia ya kuongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji msimu ujao wa ligi.


Ni mmoja wa washambuliaji hatari, mrefu na mwenye nguvu, hivyo anatarajiwa kusumbua mno mabeki wa timu pinzani.


Hafiz Konkoni - Yanga


Klabu ya Yanga imemtambulisha straika huyu juzi kutoka Bechem United ya Ghana na yeye pia akiwa ni raia wa nchi hiyo.


Amesajliwa kuchukua nafasi ya Fiston Mayele ambaye huenda wakati wowote akatambulishwa kama mchezaji wa Pyramids ya Misri.


Hata kama anaweza kuwa siyo kama Mayele, lakini kitendo cha kumaliza nafasi ya pili kwenye ufungaji bora wa Ghana msimu uliomalizika, umbile lake, urefu wake wa futi sita na inchi moja, unaweza kuwa faida kubwa sana kwake kufanya vema kwenye Ligi Kuu kama atautumia vizuri dhidi ya baadhi ya mabeki wa Kibongo wavivu wa kuruka. Tunamuweka kwenye listi hii akicheza pacha na Diao.


Willy Essomba - Simba


Wanaomuona kwenye mazoezi nchini Uturuki wanasema ni mchezaji mwenye kipaji wa cha juu na atakuwa midomoni mwa mashabiki mapema tu.


Ni mwepesi, kasi, uwezo wa kupiga chenga na kuingia kwenye eneo la adui kwa haraka sana. Ana uwezo wa kucheza winga zote mbili, lakini hapa anakaa winga ya kushoto. Pia ana uwezo wa kucheza kama namba kumi, msaidizi wa straika namba moja.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz