Yanga yampa mkono wa kwaheri mwingine - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yampa mkono wa kwaheri mwingine

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Straika wa Yanga Sc, Yusuph Athumani amejiunga na Klabu ya West Armenia ya nchini Armenia kwa mkopo wa mwaka mmoja.


Yusuph amekamilisha dili hilo ikiwa ni siku chache baada ya kumalizana mkataba wake wa mkopo wa miezi sita kwenye Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambapo alikuwa na mchango mkubwa kwa ‘Wagosi wa Kaya’ kwenye kuvuna pointi zilizowasaidia kusalia Ligi Kuu.


Ikumbukwe Yusuph alijiunga na kikosi cha Young Africans akitokea katika Klabu ya Biashara United ya mkoani Mara, akiwa sehemu ya kikosi cha kihistoria cha Klabu hiyo kilichocheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.


Uongozi wa Young Africans Sports Club umeamtakia kila la kheri Yusuph Athumani katika kipindi chote atakachokuwa kwenye Klabu ya West Armenia.


Yusuph amekuwa mchezaji wa pili kutolewa kwa mkopo baada ya David Bryson aliyejiunga kwa mkopo pia wa mwaka mmoja kwenye Klabu ya JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz