Wadau wa soka wapingana na TFF "Bingwa wa Ligi hapaswi kucheza "Play Off" ya Ngao ya Jamii" - EDUSPORTSTZ

Latest

Wadau wa soka wapingana na TFF "Bingwa wa Ligi hapaswi kucheza "Play Off" ya Ngao ya Jamii"

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Wakati michezo ya Ngao ya Jamii ikitarajiwa kushirikisha timu nne na itaanza kutimua vumbi Agosti 9 Jijini Tanga.


Baadhi ya wadau wa Soka wametoa maoni yao kuhusiana na mfumo mpya wa kumpata mshindi wa Ngao ya Jamii kuanzia msimu ujao.


Timu nne zitashiriki ambazo ni Yanga aliebeba Ubingwa msimu ulioisha, Simba aliekamata nafasi ya pili, Azam FC waliokamata nafasi ya tatu na Singida FG waliokamata nafasi ya nne.


Simba watacheza na Singida huku Aam wakivaana na Yanga katika michezo ya Play Off kisha washindi watakutana Fainali.


Wadau wanadai kuwa hatua ya Bingwa kucheza Play Off sio jambo sahihi hata kidogo.


Kanuni inatakiwa ibadilike huku ni kumkosea heshima Bingwa wa Ligi , ninavyoona mimi Bingwa anatakiwa kufuzu ooja kwa moja kwenye Fainali ya Ngao ya Jamii,


Alafu mshindi wa pili na wa tatu ndio wacheze hiyo play Off ya Ngao ya Jamii ili wakutane na Bingwa kwenye Fainali,


Kama Bingwa wa ASFC hayupo katika nafasi tatu za Juu basi mshindi wa pili acheze na Bingwa wa ASFC ili kupata Timu itakayo cheza na Bingwa wa Ligi katika Ngao ya Jamii,


Kanuni za kucheza Ngao ya Jamii zinatokana na matokeo ya msimu uliopita hivyo Bingwa anapaswa kupewa heshima yake ya kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii Kwa msimu unaofuata.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz