Taarifa mpya kutoka Yanga ni kuhusu yaliyojiri Leo kwenye MKUTANO na waandishi wa habari - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa mpya kutoka Yanga ni kuhusu yaliyojiri Leo kwenye MKUTANO na waandishi wa habari

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Yanga imeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya NMB Tanzania katika kuongeza ufanisi wa Usajili na Masuluhisho ya kifedha kwa Wanachama na Mashabiki


Makubaliano hayo yamesainiwa leo Makao Makuu ya benki ya NMB, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisaini kwa niaba ya klabu


Kwa makubaliano hayo, Mwanachama na Shabiki wa Yanga sasa anaweza kujipatia kadi yake katika Tawi lolote la NMB nchini Tanzania


Hii ina maana hata wale ambao wako mikoani na wilayani wanaweza kujipatia kadi zao katika Matawi ya NMB


Injinia Hersi amesema makubaliano hayo yatawaongezea wigo kwa Wanachama na Mashabiki wao kujisajili kwa urahisi


Makubaliano hayo pia yanakwenda mpaka kwenye eneo la miundombinu ambapo Yanga inatarajiwa kujenga uwanja wake eneo la Kaunda, NMB watakuwa washirika


Yanga pia itakwenda kusaini mkataba kama huo na benki ya CRDB



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz