Simba kuzindua jezi juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba kuzindua jezi juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Simba SC imesema kwamba ijumaa ya wiki ijayo yaani Julai 21 siku ya Ijumaa watazindua jezi yao rasmi ya msimu ujao wa 2023/24.


Kubwa zaidi na la kushangaza ambalo halijawahi kutokea ni kuwa Simba itazindua jezi hiyo katika kilele cha Mlima mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro.


Akizungumza leo Julai 15, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Imani Kajula amesema


"Nawambia rasmi hapa kwamba jezi ya Simba itazinduliwa juu ya Mlima Kilimanjaro


Jezi itaanza kupandishwa mlimani siku ya Jumatano na watakuwa kileleni siku ya Ijumaa na Jumamosi jezi itakuwa kwenye maduka yote nchini."


"Ijumaa saa 1:00 usiku jezi itakuwa imefika kileleni kwenye Mlima Kilimanjaro. Itazinduliwa na itaonekana rasmi siku hiyo."


Kauli hiyo kutoka kwa Klabu ya Simba inashusha presha kwa Mashabiki waliokuwa wanataka kujua tarehe rasmi ya upatikanaji wa jezi za Simba.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz