Namba 6 ataitikisa nchi, atambulishwa saa 6 na dakika 6 - Ally Kamwe - EDUSPORTSTZ

Latest

Namba 6 ataitikisa nchi, atambulishwa saa 6 na dakika 6 - Ally Kamwe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema utambulisho wa kiungo Jonas Mkude sio yule namba sita ambaye wamemzungumza kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa


Kamwe amesema namba sita atakuwa mchezaji wa mwisho kutambulishwa mapema wiki ijayo ambapo amebainisha kuwa utambulisho wake utaitikisa nchi


"Tutamtambulisha saa 6 na dakika 6 usiku, tunataka tukio hili liwe kama sherehe za maadhimisho ya Mwaka mpya"


"Baada ya utambulisho wake mashabiki wa Yanga wataingia mtaani kusherehekea ujio wa mchezaji huyu mkubwa lakini kuna wengine watahuzunika sana"


"Yaani siku hiyo kwa furaha ambayo Wananchi watapata, mafataki yatapigwa, ngoma zitapigwa, nyimbo zitaimbwa kila pande ya nchi hii watu watafurahi"


"Baada ya utambulisho wake, kesho yake asubuhi atakuwa hapa Makao Makuu ya CRDB ambao mashabiki wa Yanga watapata nafasi ya kuwa wa kwanza kupiga nae picha baada ya kujiunga kuwa Wanachama au kulipia kadi zao za uwanachama au shabiki," alisema KamweDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz